\v 3 Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake. \v 4 Kwa kuwa Yohana alimwambia, "Si halali kumchukua yeye kuwa mke wake." \v 5 Herode angemwua lakini aliwaogopa watu kwa sababu walimwona Yohana kuwa nabii.