sw_act_text_ulb/15/01.txt

1 line
325 B
Plaintext

\v 1 Watu fulani walishuka kutoka Uyahudi na kuwafundisha ndugu, wakisema, "msipotahiriwa kama desturi ya Musa, hamwezi kuokolewa." \v 2 Wakati Paulo na Barnaba walipokuwa na mapambano na mjadala pamoja nao, ndugu waliamua kwamba Paulo, Barnaba, na wengine kadhaa waende Yerusalem kwa mitume na wazee kwa ajili ya swali hili.