sw_1pe_text_ulb/01/11.txt

1 line
557 B
Plaintext

\v 11 Walitafuta kujua ni aina gani ya wokovu ambao ungekuja. Walitafuta pia kujua ni muda gani Roho wa Kristo aliye ndani yao alikuwa anazungumza nini nao. Hii ilikua inatokea wakati alipokuwa anawaambia mapema kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ambao ungemfuata. \v 12 Ilifunuliwa kwa manabii kwamba walikua wanayatumikia mambo haya, na si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu - masimulizi ya mambo haya kupitia wale wanaoleta injili kwenu kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni, mambo ambayo hata malaika wanatamani kufunuliwa kwake.