|
\v 19 Tunda langu ni bora kuliko dhahabu, bora hata kuliko dhahabu safi. \v 20 Ninazalisha kilicho bora kuliko fedha safi. Natembea katika njia ya haki, \v 21 katika mapito ambayo huelekea kwenye haki, ili niwape urithi wale wanaonipenda na kuzijaza hazina zao. |