\v 17 Yeye ambaye anakuwa na hasira kwa haraka hufanya mambo ya kipumbavu, na mtu anayefanya hila mbaya huchukiwa. \v 18 Wajinga hurithi upumbavu, lakini watu wenye hekima wamezingirwa kwa maarifa.