\v 24 Anayemwambia mwenye hatia, " Wewe upo sawa," atalaaniwa na watu na mataifa yatamchukia. \v 25 Bali wenye kuwakemea waovu watakuwa na furaha na zawadi za wema zitakuja kwao.