\v 25 Mtu mwenye tamaa huchochea mafarakano, bali anayemtumaini Yehova atafanikiwa. \v 26 Yule anayeutumaini moyo wake mwenyewe ni mpumbavu, bali anayekwenda kwa hekima atajilinda mbali na hatari.