\v 9 Mwanga wa mtu atendaye haki hufurahia, bali taa ya waovu itazimika. \v 10 Kiburi huzaa mafarakano, bali kwa wale wasikiao shauri jema kuna hekima.