sw_neh_text_reg/09/26.txt

1 line
377 B
Plaintext

\v 26 Basi hawakukutii na wakawaasi. Walitupa sheria yako nyuma ya migongo yao. Waliwaua manabii wako waliowaonya wakurudie wewe, nao wakafanya ukatili mkubwa. \v 27 Kwa hiyo ukawatia mikononi mwa adui zao, aliyewatesa. Na wakati wa mateso yao, walikulilia na wewe uliwasikia kutoka mbinguni na mara nyingi ukawaokoa katika mikono ya adui zao, kwa sababu ya huruma zako nyingi.