sw_neh_text_reg/13/25.txt

1 line
612 B
Plaintext

\v 25 Nami nikawasiliana nao, na mimi niliwaadhibu, na nikawapiga baadhi yao na kuvuta nywele zao. Naliwaapisha kwa Mungu, nikisema, Msiwape wana wao binti zenu, wala msiwachukue binti zao kwa ajili ya wana wenu, wala ninyi wenyewe. \v 26 Je, Sulemani mfalme wa Israeli hakufanya dhambi kwa sababu ya wanawake hawa? Miongoni mwa mataifa mengi hapakuwa na mfalme kama yeye, na alipendwa na Mungu wake. Mungu akamfanya awe mfalme juu ya Israeli wote. Hata hivyo, wake zake wa kigeni walimfanya atende dhambi. \v 27 Je, tunapaswa kukusikiliza na kufanya uovu huu hata kumhalifu Mungu wetu na kuwaoa wanawake wageni?