sw_neh_text_reg/13/01.txt

1 line
428 B
Plaintext

\v 1 Siku hiyo walisoma Kitabu cha Musa katika masikio ya watu. Ilionekana imeandikwa ndani yake kwamba hakuna Mwamoni au Mmoabu anapaswa kuja katika kusanyiko la Mungu, milele. \v 2 Hii ilikuwa kwa sababu hawakuja kwa watu wa Israeli na mkate na maji, bali walikuwa wamemwajiri Balaamu kulaani Israeli. Hata hivyo, Mungu wetu aligeuza laana kuwa baraka. \v 3 Mara tu waliposikia sheria, waliwatenga Israeli toka kwa kila mgeni.