sw_neh_text_reg/05/06.txt

1 line
509 B
Plaintext

\v 6 Nilikasirika sana niliposikia kilio chao na maneno haya. \v 7 Kisha nikafikiri juu ya hili, na kuleta mashtaka dhidi ya wakuu na viongozi. Nikawaambia, "Ninyi mnatafuta riba, kila mmoja kutoka kwa ndugu yake mwenyewe." Nikawakutanisha kusanyiko kubwa juu yao \v 8 na kuwaambia, "Sisi, kwa kadiri tulivyoweza, tumewakomboa toka utumwani ndugu zetu wa Kiyahudi ambao walikuwa wameuzwa kwa mataifa, lakini hata mnawauza ndugu na dada zenu ili wauzwe tena kwetu!" Walikuwa kimya na hawakupata neno la kusema.