sw_neh_text_reg/01/06.txt

1 line
410 B
Plaintext

\v 6 Sikiliza maombi yangu na fungua macho yako, ili uisikie sala ya mtumishi wako kwamba sasa nasali mbele yako mchana na usiku kwa ajili ya watu wa Israeli watumishi wako. Mimi ninakiri dhambi za watu wa Israeli, ambazo tumefanya dhidi yako. Wote mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi. \v 7 Tumefanya uovu sana juu yako, na hatukuzingatia amri, sheria, na hukumu ambazo ulimwamuru mtumishi wako Musa.