sw_job_text_reg/14/10.txt

1 line
343 B
Plaintext

\v 10 Lakini mwanadamu hufa; yeye huwa dhaifu; haswaa, mwanadamu hukoma kupumua, na tena yuko wapi yeye? \v 11 Kama maji yanavyopotea kutoka ziwani, na kama vile mto upotezavyo maji na kukauka, \v 12 vivyo hivyo watu hulala chini na hawaamki tena. Mpaka pale mbingu zitakapokuwa hazipo tena, hawataamka wala kuamshwa kutoka katika kulala kwao.