sw_job_text_reg/06/14.txt

1 line
451 B
Plaintext

\v 14 Kwa mtu ambaye yu karibu kuzirai, inapasa uaminifu uonyeshwe na rafiki zake; hata kwake yeye aachaye kumcha Mwenyezi. \v 15 Lakini ndugu zangu wamekuwa waaminifu kwangu kama mkondo wa maji jangwani, mfano wa mifereji ya maji ipitayo mpaka pasipo kitu, \v 16 ambayo imekuwa mieusi kwa sababu ya barafu juu yake, na kwa sababu ya theluji ambayo hujificha yenyewe ndani yake. \v 17 Wakati zikiyeyuka, hutoweka; kukiwa na joto, hutoweka mahali hapo.