sw_job_text_reg/31/13.txt

1 line
342 B
Plaintext

\v 13 Ikiwa nilikataa ombi la haki kutoka kwa watumishi wangu wa kiume na wa kike wakati walipohojiana nami, \v 14 kisha nini basi ningefanya wakati Mungu anapoinuka ili kunishitaki mimi? Atakapokuja kunihukumu, nitamjibuje? \v 15 Je yeye aliyenifanya mimi tumboni hakuwafanya wao pia? Je yeye si yeye yule aliyetuumba sisi wote katika tumbo?