sw_job_text_reg/01/16.txt

1 line
449 B
Plaintext

\v 16 Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mjumbe mwingine pia na kusema, "Moto wa Mungu umeanguka toka mbinguni na kuwateketeza kondoo na watumishi. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari." \v 17 Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mjumbe mwingine pia na kusema, "Wakaldayo walifanya vikundi vitatu, wakawashambulia ngamia, na kuondoka nao. Kwa wale watumishi, wamewaua kwa makali ya upanga. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari."