sw_job_text_reg/01/13.txt

1 line
375 B
Plaintext

\v 13 Ilitokea siku moja, wana wake wa kiume na binti zake walipokuwa wakila na kunywa mvinyo nyumbani mwa ndugu yao mkubwa. \v 14 Mjumbe akamfikia Ayubu na kusema, "Hao maksai walikuwa wakilima na punda walikuwa wakichunga karibu nao. \v 15 Wakatokea Waseba wakatuvamia na kutoweka nao. Pia wamewauwa watumishi, kwa makali ya upanga. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari."