sw_job_text_reg/01/06.txt

1 line
469 B
Plaintext

\v 6 Kisha ilikuwa siku ambayo watoto wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA. Shetani pia akaenda pamoja nao. \v 7 BWANA akamuuliza Shetani, "Umetoka wapi wewe?" Kisha Shetani akamjibu BWANA na kusema, "Natoka kuzunguka zunguka duniani, kutembea huku na huko humo." \v 8 BWANA akamuuliza Shetani, "Je unamfikiriaje mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hakuna mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu."