sw_job_text_reg/01/01.txt

1 line
393 B
Plaintext

\c 1 \v 1 Kulikuwa na mtu katika nchi ya Usi jina lake Ayubu; na Ayubu alikuwa mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na \v 2 uovu. Wakazaliwa kwake watoto saba wa kiume na mabinti watatu. \v 3 Alimiliki kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia moja za maksai, na punda mia tano na idadi kubwa ya watumishi. Mtu huyu alikuwa mtu tajiri kati ya watu wote wa mashariki.