sw_job_text_reg/42/07.txt

1 line
750 B
Plaintext

\v 7 Ilitokea baada ya kuwa amekwisha kusema maneno hata kwa Ayubu, Yahweh alimwambia Elifazi Mtemani, " Ghadhabu yangu imewaka dhidi yako na dhidi ya marafiki zako wawili kwa kuwa hamkusema maneno ya haki juu yangu kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. \v 8 Sasa basi, jitwalieni mafahari saba na mabeberu saba, kisha mmwendee mtumishi wangu Ayubu na mtoe sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yenu. Ndipo Mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi, nami nitayapokea maombi yake, ili kwamba nisiwashughulikie sawasawa na upumbavu wenu. Maana hamkusema mambo ya haki juu yangu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu." \v 9 Basi Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi na Zofari Mnaamathi walienda na kufanya kama vile Yahweh alivyowaamuru, na Mungu alimtakabali Ayubu.