sw_job_text_reg/10/04.txt

1 line
311 B
Plaintext

\v 4 Je wewe una macho ya kimwili? Je wewe unaona kama mtu aonavyo? \v 5 Je siku zako ni kama siku za wanadamu au miaka yako ni kama miaka ya watu, \v 6 hata ukauliza habari za uovu wangu na kuitafuta dhambi yangu, \v 7 ingawa wewe wafahamu mimi sina kosa na hapana mwingine awezaye kuniokoa mimi na mkono wako?