\v 7 Ni Mungu yule yule ambaye huliamuru jua lisichomoze, nalo halichomozi, na ambaye huzihifadhi nyota, \v 8 ambaye peke yake ni mwenye kupanua mbingu na kuyatuliza mawimbi ya bahari, \v 9 ambaye huumba Dubu, Orioni, kilima, na makundi ya nyota ya kusini.