\v 21 Kwa kuwa macho ya Mungu yako juu ya njia za mtu; anaziona hatua zake zote. \v 22 Hakuna giza, wala hakuna weusi mzito ambao watenda mabaya wanaweza kujificha wao wenyewe. \v 23 Kwa kuwa Mungu hahitaji kumchunguza mtu zaidi; wala hakuna haja kwa mtu yeyote kwenda mbele zake kwa hukumu.