\v 10 Basi nisikilizeni mimi, enyi watu wenye ufahamu: na iwe mbali na Mungu kwamba atatenda uovu; \v 11 na iwe mbali na Mwenye enzi kwamba atatenda dhambi. Kwa kuwa humlipa mtu kutokana na kazi yake; na humfanya mtu apate thawabu za njia zake mwenyewe. \v 12 Kwa hakika, Mungu hatendi uovu, wala Mwenye nguvu hajaIpotosha haki.