\v 15 Hainunuliwi kwa dhahabu; wala hailinganishwi na fedha. \v 16 Haiwezi kuthamanishwa na dhahabu ya Ofiri, kwa jiwe jeusi la thamani au johari. \v 17 Dhahabu na fuwele hailingani nayo kwa thamani; wala haiwezi kubadilishwa kwa vito vya dhahabu safi.