\v 9 Mungu amenirarua mimi katika ghadhabu yake na amenitesa mimi; Yeye amenisaga mimi kwa meno yake; Adui yangu amenikazia macho yake juu yangu kama yeye anavyonirarua mimi vipande. \v 10 Watu wameachama na midomo iliyowazi juu yangu; wamenipiga mimi katika shavu kwa kunitukana; wamekusanyika pamoja kinyume changu mimi.