\v 15 Ndipo kwa hakika ungeinua juu uso wako bila ishara ya aibu; Ni dhahiri, ungethibitika na usingeogopa. \v 16 Wewe ungesahau mateso yako; ungeyakumbuka hayo tu kama maji ambayo yametiririka mbali. \v 17 Maisha yako yangekuwa angavu kuliko adhuhuri; japokuwa kulikuwa na giza, litakuwa kama asubuhi.