\v 8 Wanalowanishwa na mvua ya milimani; wanalala pembeni mwa miamba mikubwa kwani hawana makao. \v 9 Lakini kuna waovu wanaowapokonya yatima katika kifua cha mama zao, na waovu wawachukuao watoto kama dhamana kutoka kwa masikini. \v 10 Lakini masikini wanatembea uchi; wajapokaa na njaa, wanawabebea wengine chakula.