sw_jas_text_ulb/03/05.txt

1 line
328 B
Plaintext

\v 5 Vivyo hivyo, ulimi ni kiungo kidogo cha mwili, lakini hujisifu kwa makuu sana. Fikiria msitu mkubwa unavyoweza kuteketezwa kwa njiti ndogo ya moto! \v 6 Ulimi ni kama moto, ni ulimwengu wa uovu, umewekwa miongoni mwa viungo vya mwili wetu, ambao unaweza kusababisha tusimpendeze Mungu, na ulimi utachomwa moto wa jehanamu.