sw_heb_text_ulb/04/08.txt

1 line
432 B
Plaintext

\v 8 Kwani kama Yoshua aliwapatia pumziko, Mungu asingelisema juu ya siku nyingine. \v 9 Kwa hiyo bado kuna Sabato ya pumziko iliyotunzwa kwa ajili ya watu wa Mungu. \v 10 Kwani anayeingia katika pumziko la Mungu yeye mwenyewe pia amepumzika kutokana na matendo yake, kama Mungu alivyofanya katika yeye. \v 11 Kwa hiyo tuweni na shauku ya kuingia katika lile pumziko, ili kwamba asiwepo atakayeanguka katika aina ya uasi waliofanya.