sw_heb_text_ulb/11/23.txt

1 line
554 B
Plaintext

\v 23 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa, alipozaliwa, alifichwa kwa miezi mitatu na wazazi wake kwa sababu walimuona kuwa ni mtoto mchanga aliyekuwa mzuri, na hawakutishwa na amri ya mfalme. \v 24 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa, alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mtoto wa binti Farao. \v 25 Badala yake, alichagua kushiriki mateso pamoja na watu wa Mungu badala ya kufurahia anasa za dhambi kwa kitambo. \v 26 Alifikiri aibu ya kumfuata Kristo kuwa ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri kwa kuwa alikaza macho yake katika zawadi ya wakati wake ujao.