sw_heb_text_ulb/12/18.txt

1 line
457 B
Plaintext

\v 18 Kwa kuwa hamkuja katika mlima ambao unaweza kuguswa, Mlima unaowaka moto, giza, kukatisha tamaa na dhoruba. \v 19 Hamkuja kwa sauti za tarumbeta, au kwa maneno yatokanayo na sauti ambayo ilisababisha kila wasikiao wasiombe neno lolote kusemwa kwao. \v 20 Kwa kuwa hawakuweza kuvumilia kile kilichoamuliwa: "Ikiwa hata mnyama agusaye mlima, lazima apigwe kwa mawe." \v 21 Ya kutisha zaidi aliyoyaona Musa alisema, "Nimeogopa sana kiasi cha kutetemeka".