sw_heb_text_ulb/11/05.txt

1 line
341 B
Plaintext

\v 5 Ilikuwa kwa imani kwamba Enoko alichukuliwa juu na hakuona mauti. "Hakuonekana, kwa sababu Mungu alimchukua" kwa vile ilinenwa juu yake kuwa alimpendeza Mungu kabla ya kuchukuliwa juu. \v 6 Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa kuwa ajaye kwa Mungu lazima aamini kwamba Mungu anaishi na kwamba huwapatia zawadi wale wamtafutao.