sw_heb_text_ulb/11/01.txt

1 line
356 B
Plaintext

\v 1 Sasa imani ni hakika aliyo nayo mtu wakati atarajiapo kitu fulani kwa ujasiri. Ni hakika ya kitu ambacho bado hakijaonekana. \v 2 Kwa sababu hii mababu zetu walithibitika kwa imani yao. \v 3 Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa amri ya Mungu, ili kwamba kile kinachoonekana hakikutengenezwa kutokana na vitu ambavyo vilikuwa vinaonekana.