sw_heb_text_ulb/10/32.txt

1 line
431 B
Plaintext

\v 32 Lakini kumbuka siku zilizopita, baada ya kutiwa kwenu nuru, ni jinsi gani mliweza kuvumilia maumivu makali. \v 33 Mlikuwa mmewekwa wazi katika dhihaka ya matukano na mateso, na mlikuwa washiriki pamoja na wale waliopitia mateso kama hayo. \v 34 Kwa kuwa mlikuwa na moyo wa huruma kwa hao waliokuwa wafungwa, na mlipokea kwa furaha adhabu ya urithi wenu, mkijua kwamba ninyi wenyewe mlikuwa na urithi bora na wa kudumu milele.