sw_heb_text_ulb/10/19.txt

1 line
447 B
Plaintext

\v 19 Kwa hiyo, ndugu, tunao ujasiri wa kuingia mahali patakatifu zaidi kwa damu ya Yesu. \v 20 Hiyo ni njia ambayo ameifungua kwa ajili yetu kwa njia ya mwili wake, mpya na hai inayopitia kwenye pazia. \v 21 Na kwa sababu tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu, \v 22 na tumkaribie na moyo wa kweli katika utimilifu wa uhakika wa imani tukiwa na mioyo iliyonyunyiziwa safi kutoka uovu wa dhamiri na kuwa na miili yetu iliyooshwa kwa maji safi.