1 line
553 B
Plaintext
1 line
553 B
Plaintext
\v 1 Kwa vile sheria ni kivuli cha mambo mema yajayo, si yale yaliyo halisi. Sheria kamwe haiwezi kuwakamilisha wale ambao wanaomkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu zilezile ambazo makuhani waliendelea kutoa mwaka baada ya mwaka. \v 2 Au vinginevyo dhabihu hizo zisingeweza kukoma kutolewa? Kwa kigezo hicho waabuduo, wakiwa wamesafishwa mara moja, wasingelikuwa na utambuzi zaidi wa dhambi. \v 3 Bali katika dhabihu hizo kuna ukumbusho wa dhambi zilizotendwa mwaka baada ya mwaka. \v 4 Kwa kuwa haiwezekani kwa damu ya mafahari na mbuzi kuziondoa dhambi. |