sw_heb_text_ulb/03/16.txt

1 line
460 B
Plaintext

\v 16 Ni akina nani hao waliomsikia Mungu na kuasi? Hawakuwa wale wote ambao Musa alikuwa amewaongoza kutoka Misri? \v 17 Na kina nani ambao Mungu aliwakasirikia kwa miaka arobaini? Siyo pamoja na wale waliotenda dhambi, ambao miili yao iliyokufa ililala jangwani? \v 18 Ni akina nani aliowaapia Mungu kwamba hawataingia katika raha yake, kama siyo wale ambao hawakumtii yeye? \v 19 Tunaona kwamba hawakuweza kuingia katika raha yake kwa sababu ya kutokuamini.