\v 25 Kwa hiyo yeye pia anaweza kwa ukamilifu kukamilisha kuwaokoa wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa kuwa yeye anaishi daima kwa kuomba kwa ajili yao. \v 26 Kwa hiyo kuhani mkuu wa namna hii anastahili kwetu. Asiye na dhambi, hatia, msafi, aliyetengwa kutoka kwa wenye dhambi, na amekuwa juu kuliko mbingu.