sw_ecc_text_reg/11/01.txt

1 line
352 B
Plaintext

\v 1 Peleka mkate wako juu ya maji, kwa kuwa utaupata tena baada ya siku nyingi. \v 2 Shiriki mkate na watu saba, hata wanane kwa kuwa haujui ni majanga gani yanayo kuja juu ya nchi. \v 3 Kama mawingu yamejaa mvua, yanajivua yenyewe chini ya nchi. Na kama mti ukianguka kuelekea kusini au kuelekea kaskazini, popote mti unapoangukia papo hapo utabakia.