sw_ecc_text_reg/06/09.txt

1 line
719 B
Plaintext

\v 9 Ni bora kuridhika na kile ambacho macho hukiona kuliko kutamani kile ambacho hamu isiyo tulia inatamani, ambayo pia ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo. \v 10 Chochote ambacho kimekuwepo, tayari kimekwisha kupewa jina lake, na vile mtu alivyo ni kama tayari amekwisha fahamika. Hivyo imekuwa haifai kugombana na yule ambaye ni muhukumu mkuu wa wote. \v 11 Maneno mengi ambayo yanaongelewa, ndivyo yasiyo na maana yanaongezeka, kwa hiyo ni faida gani iliyopo kwa mwanadamu? \v 12 Kwa kuwa ni nani ajuaye nini kilicho kizuri kwa mtu katika maisha yake wakati wa ubatili wake, siku zilizo hesabika ambazo kwa hizo anapita kama kivuri? Ni nina anayeweza kumwambia mtu kile kitakacho kuja chini ya jua baada ya kupita?