sw_deu_text_reg/17/08.txt

1 line
490 B
Plaintext

\v 8 Kama jambo linatokea ambalo ni gumu kwenu kufanya maamuzi- pengine swali la mauaji au kifo cha ajali, haki ya mtu mmoja na haki ya mtu mwingine, au swali moja la aina ya kuzulu kufanyika, au aina nyingine ya jambo-mambo ya utata ndani ya malango yenu, basi utapaswa kwenda kwenye eneo ambalo Yahwe Mungu wako atachagua kama patakatifu pake. \v 9 Utapaswa kwenda kwa makuhani, wazao wa Lawi, na kwa mwamuzi atakayetumika kwa wakati huo; mtatafuta ushauri wao, na watawapa ninyi maamuzi.