sw_deu_text_reg/16/18.txt

1 line
450 B
Plaintext

\v 18 Unapaswa kufanya waamuzi na maakida ndani ya malango yako ambayo Yahwe Mungu wako anakupa; watachukuliwa toka kila kabila, and watahukumu watu kwa hukumu ya haki. \v 19 Haupaswi kuiondoa haki kwa nguvu; haupaswi kuonyesha upendeleo wala kuchukua rushwa, kwa kuwa rushwa upofusha macho ya hekima na kupotosha maneno ya haki. \v 20 Unapaswa kufuata haki, baada ya haki peke yake, ili kwamba uishi na kurithi nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupa.