\v 23 Nitarundia maafa juu yao; nitafyatua mishale yangu yote kwao; \v 24 Watapotea kwa njaa na kumezwa kwa joto liwakalo na uharibifu mchungu; nitatuma kwao meno ya wanyama wa mwituni, pamoja na sumu ya vitu vitambaao mavumbini.