sw_deu_text_reg/23/21.txt

1 line
412 B
Plaintext

\v 21 Unapofanya kiapo kwa Yahwe Mungu wako, haupaswi kukawia kuikamilsha, kwa maana Yahwe Mungu wako hakika atadai kiapo hicho; itakuwa dhambi kwako usipokamilisha. \v 22 Lakini iwapo utajizuia kutoa kiapo, haitakuwa dhambi kwako. \v 23 Kile ambacho kimetoka kinywani mwako unapaswa kukifuata na kukitekeleza; kulingana na kiapo ulichotamka kwa Yahwe Mungu wako, chochote ulichotamka kwa hiari kwa kinywa chako.