\v 19 Hutakiwi kumkopesha Muisraeli mwenzako kwa riba – riba ya fedha, riba ya chakula, au riba ya kitu chochote kinachokopeshwa kwa riba. \v 20 Kwa mgeni unaweza kukopesha kwa riba; lakini kwa Muisraeli mwenzako haupaswi kukopesha kwa riba, ili kwamba Yahwe Mungu wako aweze kukubariki katika kila jambo uwekalo mkono wako, katika nchi ambayo mnaenda kumiliki.