sw_dan_text_reg/09/17.txt

1 line
572 B
Plaintext

\v 17 Basi sasa, Mungu wetu, sikiliza sala za mtumishi wako na maombi yake kwa ajili ya rehema; kwa ajili yako, Bwana ufanye uso wako ung'ae katika sehemu yako takatifu iliyoachwa ukiwa. \v 18 Mungu wangu, fungua masikio yako na usikie; fumbua macho yako na uone. Tumeharibiwa; utazame mji unaoitwa kwa jina lako. Hatukuombi msaada wako kwasababu ya haki yetu, ila kwasababu ya rehema zako kuu. \v 19 Bwana, sikiliza! Bwana, samehe! Bwana, tuangalie na ufanye jambo! Kwa ajili yako mwenyewe, usichelewe, Mungu wangu, kwa kuwa mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako."