\v 3 Niliugeuza uso wangu kumwelekea Bwana Mungu, ili kumtafuta yeye kwa sala na maombi, kwa kufunga, na kuvaa nguo za magunia na kukaa katika majivu. \v 4 Nilimwomba Yahweh Mungu wangu, na niliungama dhambi zetu. Nilisema, "Tafadhali nakuomba, Bwana--wewe ni mkuu na Mungu wa kuheshimiwa--ni wewe pekee utunzaye maagano na uliye mwaminifu katika kuwapenda wale wakupendao wewe na kuzishika amri zako.