sw_2ch_text_reg/09/01.txt

1 line
416 B
Plaintext

\c 9 \v 1 Malkia wa Sheba aliposikia kuhusu umaarufu wa Sulemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Akaja pamoja na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliosheheni manukato, dhahabu nyingi, na vito vingi vya thamani. Alipofika kwa \v 2 Sulemani, akamwambia yaliyokuwa moyoni mwake. Sulemani akamjibu maswali yake yote; hakuna kitu kilichokuwa kigumu sana kwa Sulemani; hakuna swali ambalo hakulijibu.